HISTORIA YA BUWASA

 

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bukoba (BUWASA) inahudumia Kata 14 zilizopo katika Manispaa ya Bukoba, na pia kupitia Tangazo la Serikali Na.214 la tarehe 26 Februari 2021, BUWASA iliongezewa maeneo ya kutoa huduma ambayo ni Karagwe (Kayanga-Omurushaka), Missenyi (Kyaka-Bunazi na Mutukula), Bukoba Vijijini (Kemondo, Maruku, Katerero, Kanyangereko, Karabagaine, Katoma na Nyakato) na mji wa Muleba katika Wilaya ya Muleba.

 

Mamlaka kwa kipindi cha miezi sita kuanzia January hadi June 2024 imeweza kukusanya kiasi cha Tzs 2,607,800,115.56 ambazo zimetumika katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya Taasisi kama utekelezaji wa miradi midogo midogo kwa fedha za ndani hususani upanuzi wa mtandao kwa kusogeza huduma karibu na wananchi,kulipa wazabuni wanaotoa huduma mbalimbali,kulipa umeme wa kuzalisha maji pamoja na mishahara ya watumishi.

Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa eneo la Manispaa ni asilimia 92 na wastani wa asilimia 79 kwa maeneo yote yanayohudumiwa na Mamlaka. Upatikanaji wa huduma ya Majisafi katika mji wa Bukoba ni kwa masaa 24 iwapo hakuna tatizo lolote kwenye chanzo. Kwa sasa tunaendelea na utekelezaji wa Mradi wa upanuzi wa mtandao awamu ya pili katika Manispaa ya Bukoba ambao kwa sasa upo asilimia 80 ya utekelezaji na tunategeme ukamilike ifikapo Aprili 2024.  Mradi huu ukikamilika utaongoze hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kufikia asilimia 100 kwa mji wa Bukoba na tutakuwa tumetekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa asilimia 100 ya kuhakikisha hali ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa maeneo ya mjini inafikia Zaidi ya asilimia 95 ifikapo 2025

Katika jitihada za kuongeza wateja, Mamlaka inaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi June 2024 kama inavyoonekana katika jedwali hapa chini.