Namna ya kuomba huduma ya maji

  • Mteja afike Ofisi za Huduma kwa Mteja kwa ajili ya kufanya maombi na kuingizwa kwenye mfumo, akiwa na picha moja ya passport pamoja na kitambulisho kimoja wapo kati ya cha mpiga kura, NIDA au leseni ya udereva. 
  • Baada ya kujiandikisha Wataalam wa Mamlaka watafanya ukaguzi (survey) kwenye eneo/nyumba inayoombewa huduma ya maji na kutayarisha gharama.
  • Mteja atapata taarifa ya ukaguzi na gharama za kuungiwa maji ndani ya siku nne (4) kuanzia tarehe aliyofanya maombi ya huduma kupitia simu yake ya mkononi.
  • Gharama zote zinazohusika zikiwemo za vifaa zitalipwa na mteja kupitia malipo ya Serikali (control number) kwa njia ya TIGO PESA, HALOPESA, MPESA, AIRTEL MONEY pamoja na T-PESA na kwa njia ya Mabenki na mawakala wa CRDB, NMB, NBC na TCB.